Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize kuiwakilisha Afrika Mashariki tuzo za MTV Europe Music Awards 2019

78184 Pic+hamionize

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. “Sipo tayari kufanya mahojiano kwa sasa, kuna vitu vingi juu yangu vinaendelea ikiwamo kutajwa kwenye tuzo, nikiwa tayari kwa hilo nitakuambia” amejibu kwa kifupi msanii Harmonize.

Harmonize amejibu hayo leo Jumatano Oktoba 2, 2019 alipotakiwa kufafanua kuhusu alichopost kwenye mtandao wa Instagram kuwa anataka kuachia wimbo mpya hivi karibuni.

Staa huyo aliyeomba kuondoka kwenye lebo ya WCB ambayo aliingia nao mkataba wa zaidi ya miaka 10, siku za hivi karibuni amekuwa hasikiki kwenye vyombo vya habari zaidi ya kuachia nyimbo mbili za kushirikishwa nje ya lebo hiyo zikiwamo ‘Inabana’ aliyofanya na Eddy Kenzo na ‘Oyoyo’ aliyoshirikishwa na Skales.

Kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards  2019, msanii Harmonize mshiriki pekee kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki kuwania tuzo ya Best African Act.

Kwenye tuzo hiyo anapambana na wasanii kama Burna Boy, Teni, Nasty C, PrinceKaybee na Toofan kutoka Afrika Magharibi.

Tuzo hizo zinatarajia kufanyika Novemba 3, 2019 jijini London.

Pia Soma

Advertisement
Pamoja na wasanii kutoka Afrika, Harmonize atapata bahati ya kutumia jukwaa moja na mastaa kama Ariana Grande, ‘Thank u, nex’  Billie Eilish, ‘Bad guy’ Lil Nas X, ‘Old Town Road (Remix)’ Rosalia, J Balvin, ‘Con Altura’ na Taylor Swift, ‘ME!’ ambao wanawake kipengele cha video bora.

Kipengele kingine kitakachowaniwa siku hiyo ni msanii bora wa mwaka ambapo Harmonize atawashuhudia kina Ariana Grande, J Balvin, Miley Cyrus, Shawn Mendes na Taylor Swift wakichuana.

Katika orodha hiyo msanii ambaye ametajwa mara nyingi ni Ariana Grande ambaye ametajwa kwenye vipengele sita kikiwamo cha video bora, wimbo bora, Pop bora, mwimbaji bora wa laivu na msanii mwenye mashabiki wengi.

Chanzo: mwananchi.co.tz