Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize kufanya balaa zito tamasha la Singida Big Star

Harmonize Pic Data.png Harmonize kufanya balaa zito tamasha la Singida Big Star

Thu, 4 Aug 2022 Chanzo: Habari Leo

Mkurugenzi wa lebo ya Konde Worldwide, Abdul Kahali ‘Harmonize’ amesema kuwa amefurahi baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha la Singida Big Stars, ni jambo la heshima kwake na mashabiki wasubiri kushuhudia historia ikiandikwa mkoani humo.

Harmonize atatumbuiza wakati Singida Big Stars, watakapokuwa wakiwatangaza wachezaji wao wapya na baadae kufuatiwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Alisema kuwa ni jambo kubwa kuaminiwa na timu ya Singida Big Stars, ambayo licha ya kuwepo wasanii wengi hapa nchini lakini wamempa yeye nafasi hiyo ya kutumbuiza na kusisitiza hawajakosea kufanya hivyo kwani anaenda kuandika historia ya mkoani Singida.

“Watu wangu wa Singida, kaeni tayari kwa onyesho la kihistoria, naamini hakuna mtu ambaye atajutia kuja kwenye siku hii ya Singida Big Stars, burudani itakayotolewa hapo ni ya viwango vya juu sana.”

“Sitaki kuwa muongeaji sana tukutane uwanjani tufurahie muziki mzuri na tuwashuhudie wachezaji wetu wapya huku tukiiunga mkono timu yetu ya nyumbani,” alisema Harmonize.

Chanzo: Habari Leo