Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize kuachana na wasanii wake Konde Gang?

Konde Gang Nm Konde Gang

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lebo ya Konde Music Worldwide inatarajiwa kuwapa mkono wa kwaheri baadhi ya wasanii wake hapo Oktoba 10 wanapotimiza miaka minne.

Lebo hiyo yake Harmonize inasimamia wasanii kama Ibraah, Anjella, Killy na Cheed.

Ujumbe huo ameutoa Harmonize kupitia Insta Story. Mwimbaji huyo ameandika;

Tarehe 10/10 Konde Gang tunatimiza miaka minne sio rahisi, asikuambie mtu vipindi vya kuchekeka kulia kuteleza na kuamka yote kwa yote tunashukuru Mungu pamoja na wewe unayesoma.

Umeifanya Konde Gang kuwa Lebo kubwa Afrika Mashariki, asante sana lengo ni kujikwamua kama watoto wa kimaskini.

Tunatarajia kufanya jambo kubwa katika siku hiyo kubwa kwetu ikiambatana na kuhitimu baadhi ya members kadhaa wa Konde Music.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live