Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize huwenda akamtangaza Sallam kama meneja wake mpya

Harmo Na Mendez Harmonize huwenda akamtangaza Sallam kama meneja wake mpya

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjini ukikosa tu bando unapitwa na mambo! Kuna taarifa za chinichini zinadai huwenda staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul 'Harmonize' akamtangaza, Sallam SK kama meneja wake mpya.

Hiyo inakuja kukiwa na taarifa za Harmonize kuachana na meneja wake Kajala Masanja ambaye mbali na umeneja alikuwa mpenzi wake na penzi limeshaota mbawa.

Kupitia Insta Story kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ametangaza kuwa anakwenda kumtambulisha meneja wake mpya, Desemba 25, 2022.

"Woow!! 25 suprise artist+new manager. Dont miss this big night in the game @harmonight2022 tickets out tomorrow...my new manager 2.m table reserved 25 December will be night to remember," aliandika Harmonize.

Mpaka sasa Harmonize mwenyewe hajamweka wazi ni nani huyo anakwenda kumtangaza siku hiyo kama meneja wake mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live