Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu msanii Harmonize atuonyeshe kwenye mitandao ya kijamii kuwa yuko Zanzibar kwa ajili ya kushuti video ya baadhi ya nyimbo zake, taarifa aliyoitoa #Harmonize leo ni kuwa amezuiwa na Baraza la Sanaa la Zanzibar kufanya video Zanzibar katika mwezi huu mtukufu wa Ramdhan.
Katika video mbalimbali zinazosambaa mtandaoni zinamuonyesha Harmonize akiomba radhi kwa Wazanzibar kama kuna usumbufu wowote aliowasababishia.
Harmo ameweka wazi kuwa hakusikia tangazo kutoka serikali ya Zanzibar kuhusu katazo la kushuti video kwenye kipindi cha mwezi huu mtukufu wa Ramadhan japo anasema alikaribia kumaliza kuzishuti video hizo.