Staa wa Muziki Harmonize anasema huwenda zile siku alizojiwekea kukaa bila kufanya mapenzi (siku 30) zikaongezeka kwani anayempenda kuna Mwamba anajifanya anampenda zaidi yake.
Kupitia kwenye komenti za Instagram, Harmonize ametoa kauli hiyo alipokuwa akimjibu mwanaye anayefahamika kwa jina la Sam cha Upole ambaye aliandika kuwa, anamhesabia Harmonize kama anaweza kutimiza siku thelathini kweli bila kukutana na mwanamke.
"Nipo sana ninayempenda nahisi kuna mtu anajifanya anampenda kunizidi so nimekaa pale namwangalia ataishia wapi nianzie hapo. Mnanijua family nikishapendagaa eti mimi huyu huyu," aliandika Harmonize.