Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize aweka utimu pembeni, amvulia kofia Abdukiba

Abdukiba Harmo Harmonize na Abdu Kiba

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki iliyopita kituo cha habari cha Clouds Media lilikuwa na tamasha la Fiesta mkoani Mtwara ambako ni nyumbani kwa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Harmonize.

Wakati wa Tamasha hilo, Msanii Abdukiba kutoka rekodi Lebo ya Kings Music ya inayomilikiwa na kaka yake Alikiba alikuwa miongoni mwa wasanii waliopanda jukwaani na kutumbuiza.

Abdukiba aliwashangaza wengi alipoimba wimbo mpya wa Harmonize, Amelowa. Baadaye katika mahojiano na wanahabari, Abdukiba alisema kwamba alilazimika kuimba wimbo wa Harmonize nyumbani kwao kama njia moja ya kumfagilia na kuutambua mchango wake katika Sanaa ya muziki wa Bongo Fleva, na pia kumtambua kama mfalme nyumbani kwao Mtwara.

“Naweza nikasema kwamba ninakubali kazi zake ambazo anafanya, zinaonekana, anajituma na kupambana na pia anaonesha anataka kuipeleka nchi sehemu gani,” Abdukiba alijibu sababu yake kuimba wimbo wa Harmonize.

Pia alisema kwamba licha ya hayo, anaupenda wimbo huo kwa kile alisema kuwa una mawazo fulani ambayo yanajiradidi katika kichwa chake.

Baadae kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, aliposti kipande hicho akiimba wimbo wa Harmonize jukwaani na cha ajabu ni kwamba kwa mara ya kwanza Harmonize aliweka utimu pembeni na kumvulia kofia Abdukiba, huku akionekana kufurahia kitendo chake kumtambua nyumbani kwao Mtwara.

“Noma sana mzee wangu, ”Harmonize aliandika kwenye video hiyo ya Abdukiba, huku msanii huyo naye pia akimwekea emoji ya upendo na kuifuatisha na nyingine ya taji kama njia moja ya kumkubali kimuziki."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live