Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize awatolea povu wanaomsema anaendeshwa na mapenzi

Harmonize Afunguka Wasanii Kupewa Magari Kwenye Lebo Harmonize

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva Harmonize amewatolea uvivu wanaodai kuwa anamawazo ya mapenzi, amesema katika ma-ex wake hakuna wa kumfanya alewe.

#Konde amefunguka hayo kupitia Instastory yake na kueleza kuwa ana kila kitu katika maisha yake mafanikio, ndugu, mtoto, nyumba, magari na hata pesa hivyo siyo mbaya kwake kunywa pombe maana kwa upande wake ni burudani.

Aidha #Harmonize ameweka wazi kuwa ameeleza hayo kwa sababu ameanza kuona comment za watu wakidai kuwa anakunywa sana pombe kwa sababu ya mawazo ya mapenzi, ametengua kauli hiyo na kusema kuwa ma-ex wake wote ni washikaji wake na ni suala la maamuzi tuu arudi kwa ex gani maana hakuna wa kumfanya alewe.

Ikumbukwe Harmonize aliwahi kumvisha pete muigizaji maarufu nchini #Kajala na mahusiano yao kuishia kati baada ya wawili hao kugombana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live