Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize atoa ya moyoni "Kundesha Lebo sio kazi rahisi"

Winner Harmo Harmonize atoa ya moyoni

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize au Konde Boy; ni staa mwingine mkubwa wa muziki nchini Tanzania ambaye anasema kuwa, kuna wanapenda kumchukulia poa yeye na lebo yake ya Konde Gang, lakini ukweli ni kwamba amejitahidi na anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kufanya mambo makubwa na kuwasaidia vijana wengine ili nao wasaidie familia zao.

Akizungumza hivi karibuni, Harmonize au Harmo alisema; “Watu wasinichukulie poa, najitahadi kufanya vitu kwa uwezo wangu wote ili kusaidia wengine, nao wasaidie familia zao.”

Kumbuka, Harmonize na lebo yake ya Konde Gang imewatoa wasanii Ibraah na Anjella ambao kabla ya hapo walikuwa hawajulikani kabisa, lakini sasa ndani nan je ya Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live