Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize aondoa kesi ya picha za uchi dhidi ya Kajala na bintiye

1988a89c8e194c44 Harmonize aondoa kesi ya picha za uchi dhidi ya Kajala na bintiye

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Muimbaji Mtanzania Harmonize ameondoa kortini kesi dhidi ya mpenzi wake wa zamani Kajala na binti yake PaulaWawili hao walikuwa miongoni mwa washukiwa waliokamatwa kufuatia madai ya kusambaza picha za uchi zinazodaiwa kuwa za muimbaji huyo mtandaoniHarmonize alitengana na Kajala baada ya kudaiwa kumnyemelea Paula

Afisa Mkuu Mtendaji wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize ameondoa kortini kesi dhidi ya mpenzi wake wa zamani Kajala na binti yake Paula.

Muimbaji huyo aliyevuma na wimbo Happy Birthday alikuwa amewashtaki wawili hao kwa kufuja picha zake chafu mtandaoni.

Mnamo Aprili 20, 2021, Kajala, ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu za Bongo na binti yake Paula walikamatwa na kuhojiwa.

Kisha baadaye waliachiliwa na dhamana kwa kusambaza picha chafu ambazo zinadaiwa zilikuwa za Harmonize.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kisa hicho, Harmonize aliambia jarida la Ijumaa kuwa amezika yote hayo katika kaburi la sahau.

"Tayari nimeamua kuwasamehe Kajala na Paula kwa sababu sitaki kesi zozote za korti. Nimefanya uamuzi huo kwa hivyo maisha yanasonga mbele. Hivyo sitaki tena kusikia lolote kuhusu suala hilo," alisema.

Je Kajala na Harmonize watarudiana?Isitoshe, Harmonize aliulizwa endapo anapanga kurudiana na Kajala, lakini aliruka swali hilo na badala yake kusema:

"Nimesema nimewasamehe na ndio maana nilifuta kesi hiyo, Sina shida na yeyote."

Kamanda wa polisi wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alifichua kwamba Kajala na Paulawalikamatwa na usiku wa Jumanne, Aprili 20, punde walipotua wakitokea Dubai.

Walikamatwa pamoja na wanamuziki Rayvanny na Baba Lao

“Ni kweli tumemkamata Kajala na Paula tukawahoji baada ya mlalamikaji Harmonize kuleta malalamiko kituoni lakini tayari tumeshawaachia kwa dhamana,” alisema kamanda huyo.

Harmonize na Kajala walianza kuchumbiana miezi michache iliyopita, na mtandao wa kijamii ulikuwa umepambwa na picha zao za mahaba.

Hata hivyo mapenzi yao hayakudumu huku Rayvanny akimtuhumu Harmonize kujaribu kulala na Kajala na Paula.

Rayvanny alimtuhumu Harmonize kwa kumtumia binti ya Kajala, Paula utupu wake na kushusha heshima yake katika jamii.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke