Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize anampindulia meza Diamond na kuzivunja

FcWE Harmonize anampindulia meza Diamond na kuzivunja

Fri, 25 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Kwa namna Harmonize anavyopindua hizo meza za Diamond Platnumz waweza kusema anafanya uchokozi wa makusudi, lakini ikiwa hadi anazivunja kabisa huo si uchokozi? Hapana! Hiyo ni burudani kwa mashabiki.

Kupinduliwa na kuvunjwa kwa meza hizo sio uchokozi. Vipande vya meza hizo ndio uwanja wao wa kuuza bidhaa yao kwa mashabiki. Wateja wanapenda kuona ushindani. Makala haya yanaenda kuangazia matukio machache kuhusiana na hilo.

Kofia ya Magufuli

Miongoni mwa mambo yaliyomuweka Diamond kwenye vichwa vya habari hivi karibuni ni pam-oja na kitendo cha kuvishwa kofia na Rais Magufuli wa-kati akitumbuiza kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza.

Hiyo ilikuwa ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Septemba 7 mwaka huu. Lakini Septemba 14, Harmonize akapindua meza kwenye Uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.

Hii ni baada ya yeye pia kuvishwa kofia na mgombea Urais Magufuli kama ilivyotokea kwa Diamond na ni aina ile ile ya kofia. Kama ni mchezo wa soka, basi hapo ubao wa matangazo ungesoma goli 1-1, lakini kwa kawaida siku zote anayesawazisha ndiye mwenye furaha zaidi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz