Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize ana ugomvi na waandaaji wa Tuzo?

Harmonize Mkl Harmonize ana ugomvi na waandaaji wa Tuzo?

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mnamo Septemba 16, 2022, waandaaji wa Tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA) waliachia orodha ya wasanii wanaowania vipengere mbalimbali vya tuzo hizo lakini jina la msanii kutoka Bongo, Harmonize halikuwepo huku mastaa wengi wa Bongo wakitajwa kwenye tuzo hizo.

Haijaishia hapo tu, jana Jumapili, Septemba 25, 2022 zilitangazwa nominations za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) ambapo pia jina la Harmonize halijaonekana popote pale.

Wadau mbalimbali wa muziki nchini wamekuwa wakihoji kwa nini Harmonize hatokei kwenye Tuzo hizo, wengine wakienda mbali zaidi na kudai kuwa huenda ana ugomvi binafsi na waandaaji wa tuzo hizo.

Ikumbukwe pia kuwa, Kiba naye amepata nomination moja kwenye Tuzo za AFRIMA wakati kwenye tuzo za AFRIMMA akishindwa kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live