Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amweka tena Kajala kwenye bango

HARMONIZE BANGO Harmonize amweka tena Kajala kwenye bango

Fri, 22 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa leo ni Julai 22, 2022 ni siku ya kuzaliwa ya muigizaji na meneja wa Harmonize, Kajala Masanja. Habari ikufikie, amewekwa tena kwenye bango!

Bango hilo ambalo wambea bado hawajajua limewekwa maeneo gani, video ambazo Kajala mwenyewe ameziposti kwenye Insta Story yake, zimemuonesha akiwa ndani ya gari na Harmonize.

Wakiwa karibu kabisa na bango hilo, Harmonize alimuonesha Kajala bango hilo, alifurahi sana huku nyuma ya gari wakisikika chawa wakimwambia Kajala asije akalia.

Hii si mara ya kwanza kwa Kajala kuwekwa kwenye bango barabarani. Harmonize aliwahi kumuweka wakati alipokuwa anamuomba msamaha ili warudiane walipokuwa wameachana.

Kajala leo Julai 22, 2022 anatimiza miaka 39 ambapo tayari amechumbiwa na Harmonize huku pia akiwa ni mama wa mtoto mmoja, Paula.

Ikumbukwe Paula alimpata enzi za ujana wake akiwa kwenye penzi zito na prodyuza P Funk kisha wakaachana na baadaye akaolewa na mwanaume mwingine kisha ndoa ikavunjika na sasa anatanua na Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live