Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amwagia Paula mamilioni ya pesa kumlainisha

Harmo Kajala Paula Harmonize, Kajala na Paula

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paula Kajala au Pau; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania ambaye aliapa kwamba labda afe ndipo mama yake, Kajala Masanja amrudie ex-wake, Harmonize, lakini sasa kibao kimegeuka.

Nyuma ya pazia, stori za ndani zinasema kuwa, baada ya Harmonize au Konde Boy Mjeshi ambaye ni msanii wa Bongo Fleva kuona Paula anaendelea na msimamo huo kwa mama yake ambaye ameshakubali kumrudia na maisha ni bambam, jamaa huyo ameamua kutumia ‘plan B’.

Harmonize au Harmo anadaiwa kumwagia Paula mamilioni ya pesa ili kumlainisha; na kama wasemavyo, hakuna uchawi mkubwa zaidi ya pesa hivyo amefanikiwa kwa sababu mrembo huyo tayari ameungana na mama yake nyumbani kwa jamaa huyo, Salasala jijini Dar na anamsalimia ‘Shikamoo Daddy’.

Sasa; stori ya ndani iko hivi; Paula muda siyo mrefu atazindua bonge la duka la nguo jijini Dar ambapo tayari fremu ya shilingi milioni nane imelipiwa na mtaji wa shilingi milioni 14 umetolewa na Harmonize.

Mtu wa karibu wa Paula amedokeza kuwa, kwa sasa Paula anapiga picha matata za mavazi za tangazo la duka hilo ambapo litaibua mjadala kwamba ni lake au siyo lake anafanya tu matangazo ili liendelee kuwa gumzo.

Inaelezwa kuwa, Harmonize kwa sasa anawamwagia pesa mama na mwanawe kwani haamini kama msamaha wake ungekubalika huku wawili hao wakiendelea kushambuliwa kwa kukubali msamaha huo.

Mwijaku; ni mtangazaji na muigizaji maarufu Bongo ambaye ni mtu wa karibu wa Harmonize akienda nyumbani kwake muda wowote ambaye anathibitisha Paula kukubali kumfuata nyumbani kwa jamaa huyo na wanainjoi maisha kwani kwa sasa mambo yapo sawa kabisa; wamesahau yaliyopita na sasa wanaganga yajayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live