Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amuombea msamaha Diamond Rwanda

Diamond Harmonize Dsf Harmonize amuombea msamaha Diamond Rwanda

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wote tunajua kuwa Harmonize yupo nchini Rwanda siku ya pili sasa tangu aende kule.

Na jana amefanya mahojiano kupitia RwandaTv na kuzungumza mengi ikiwemo kuukuza muziki wa Bongo Fleva.

Mbali na hilo Harmonize amemuombea msamaha bosi wake wa zamani, Diamond Platnumz kwa Wanyarwanda kwa kutokufanya show kule.

Ikumbukwe Diamond alitarajiwa kwenda kufanya show katika Arena ya Kigali kabla ya mwaka mpya na aliweka wazi sababu za kutohudhuria show ile akisema kuwa walipishana na waandaaji wa Show ile ingawa Diamond alikuwa tayari kufanya show na alisema lazima akafanye show Rwanda.

Kutokana na tukio hilo, HarmonizE ameamua kumuombea msamaha Diamond na kusema hakujua shida ilikuwa nini ila anamuombea msamaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live