Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amuombea msaada Haitham Kim

Harmonize Amuombea Msaada Haitham Kim Harmonize amuombea msaada Haitham Kim

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva Rajabu Abdul 'Harmonize' ametumia sekunde kadhaa kumuombea msanii wa kike Haitham Kim ambaye amelazwa ICU.

Akiwa visiwani Zanzibar usiku wa kuamkia leo Agosti 31, 2023, Harmonize aliomba mashabiki wasimame kwa sekunde kadhaa kumuombea msanii huyo anayepigani uhai wake lakini kuwaomba viongozi wa nchi kufikisha ujumbe huo kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Viongozi najua mpo hapa, naomba tumuombe mama yetu tunafahamu amejaliwa rehema, amsaidie msanii mwenzetu Haitham ambaye amelazwa, ndio kwanza alikuwa anaanza na hana uwezo wa kujitibia," alisema Harmonize.

Haitham anasumbuliwa na tatizo kwenye mapafu mpaka kushindwa kupumua na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Temeke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live