Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amtungia Diamond nyimbo sita

Harmo Diamond Harmonize amtungia Diamond nyimbo sita

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya miaka minne, Konde Music imepotea katika ushindanii huo baada ya kujikuta imesalia na msanii mmoja tu ambaye ni Ibraah, huko WCB Wasafi ikiwa na wasanii wanne, Queen Darleen, Lava Lava, Mbosso na Zuchu.

Kitendo cha Konde Music kuachana na wasanii wake wa watano ndani ya muda mfupi, kinatajwa kama utakuwa ndio mwisho kwa Harmonize kushindana na Diamond au kumpunzisha katika mambo yake.

Kwani ni wazi Harmonize alikuwa amemuweka Diamond kifuani mwake tangu aondoke WCB Wasafi, nyimbo zake zimethibitisha hilo mara kadhaa, na hii ndio ilikuwa inatoa picha kuwa yupo tayari kushindana na Diamond.

Hadi sasa katika nyimbo zake sita, Harmonize amemzungumzia Diamond, iwe moja kwa moja au kwa kuzunguka, ni kama anatapika nyongo kimtindo, hizi ni nyimbo sita za Harmonize ambazo amemzungumzia Diamond.

Uno: Huu ulikuwa ni wimbo wake kwanza kuutoa tangu aachane na WCB Wasafi, ulifanya vizuri sana, huku Harmonize alimrusha Diamond pamoja na mzazi mwenziye, Zari The Bosslady.

“Uno la Chibu Chibu linamkondesha Zari” aliimba Harmonize wimbo huo licha ya wawili hao kuwa tayari wameachana, na Diamond tayari alikuwa na mahusiano na Tanasha Donna toka nchini Kenya.

Kushoto Kulia: Katika ngoma hii Harmonize anamshukuru Diamond kama miongoni mwa watu waliomleta mjini na kumpa nafasi, na kutaka choko choko zisiingizwe katika muziki wao.

“Peace kwa walionileta mjini Mondi wa Tandale, maneno majungu tupa chini muziki utawale” aliimba Konde Boy ambaye katika video ya wimbo huo anaonekana kama mtumwa aliyejeruhiwa ambaye amevunja minyororo na kuondoka zake.

Ushamba: Ukiachana na wimbo wenyewe, pia video yake iliibua gumzo kufuatia Harmonize kumtumia kijana mwenye kufanana na Diamond kwa asilimia kubwa.

“Halina meno hilo Simba Zee, likila demu lazima litangaze”, inajulikana kuwa Diamond ndiye amekuwa akitumia jina la Simba katika muziki, ukiachana na yule kijana anayefanana naye katika video, ikatoa picha kamili kijembe hicho kinaenda kwa nani hasa.

Usia: Hii ni ngoma inayopatikana kwenye albamu yake ya tatu, ‘High School’ ambayo ilitoka Novemba 2022, huku napo kampitia Diamond vilivyo, utakumbuka ngoma mbili za awali zipo katika albamu yake, Afro East.

“Simba na ukali wake wote ila akimuona Tembo anachimba, ila hiyo haimfanyi Tembo kuvimba” anaimba Harmonize ambaye amekuwa akitumia jina la Tembo katika muziki wake, huku akijichora na tattoo ya mnyama huyo mwenye nguvu za kutosha.

Wapo: Kufuatia tukio la Mama mzazi wa Diamond, Bi. Sandra maarufu kama Mama Dangote kudai kuwa Mzee Abdul Juma Issack si baba halisi wa Diamond bali ni baba mlezi, Harmonize hakulikalia kimya hilo, akatoa ngoma; Wapo.

“Mama na Baba ndio nguzo ya dunia watunze, sio Baba Dangote analia, Mama Dangote anacheka” aliimba Harmonize akiwa Zanzibar katika Mapinduzi Cup baada ya kuwepo maswali kwanini Mzee Abdul haonekani kunawiri kama baba wa Staa, ndipo Mama Dangote akaja kuweka wazi kwanini hilo lipo hivyo.

Champion Remix: Huu ni wimbo wa Kontawa uliotoka hivi karibuni ambapo Harmonize ameshirikishwa, ndani yake nipo amepita na viongozi wa WCB Wasafi, Mkubwa Fella, Babu Tale na Sallam SK.

“Nimetoboa mbele ya Mkubwa na Tale, Kipara na Asake wa Tandale,” anaimba Harmonize katika ngoma hiyo.

Sallam SK alisikia ujumbe huo na kuhoji kama Harmonize ameua lebo ya Konde Music na kuanzisha kundi (Wagambo Mtu Mbili) akiwa na Ibraah ambaye ndiye msanii pekee aliyesalia kwenye lebo hiyo.

Hata hivyo, Diamond hajawahi kutumia wimbo wake wowote kumzungumzia Harmonize jambo lilotoa picha kuwa ni Konde Boy ndiye anata ligi hiyo na sio Chibu. Na sasa baadhi ya mambo kama lebo ambayo Harmonize aliweka ndio sehemu ya kupambana na Diamond hali si shwari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live