Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amtaka Ibraah kutoa ngoma baada ya ngoma

Harmonize Ibrah Er Harmonize amtaka Ibraah kutoa ngoma baada ya ngoma

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki jana lebo ya Konde Music Worldwide ikiongozwa na CEO Harmonize waliwaaga wasanii Cheed na Killy ambao kwa taarifa zilizowekwa wazi ni kwamba mkataba wao ulikamilika.

Baadae kuliibuka na sekeseke kuwa wawili hao wameelekea katika bodi ya kusimamia Sanaa nchini Tanzania, BASATA kwa kile walimshtaki aliyekuwa bosi wao Harmonize kuwa aliikatisha mikataba yao kwa njia isiyo halali.

Katika taarifa na ambazo zilichapishwa na vyanzo vya habari, Cheed na Killy waliteta kuwa walipewa taarifa za kusitishwa mikataba yao kwa njia ya maneno hali ya kuwa waliingia mikataba na lebo ya Konde Gang kwa maandishi.

Iliarifiwa kuwa Harmonize baada ya kutakiwa kujiwasilisha mbele ya BASATA ili kupata suluhu ila hakutokea yeye pamoja na uongozi wa lebo yake, katika kile ambacho sasa kimeonekana ni mzozo wa kisheria ambao wawili hao wameanzisha na Harmonize.

Kwa upande wake, msanii Harmonize anaonekana kutotilia maanani maneno na madai ambayo wawili hao wameibua dhidi yake na badala yake ameelekeza macho katika wasanii wawili amabo alibaki nao, Ibraah na Anjella, na kuwataka kujitoa kwa nguvu kubwa kimuziki kwani sasa wamebaki wachache.

Akizungumzia hili kwenye picha za Ibraah aliyepakia akiwa na tabasamu na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kuwa na tabasamu siku zote, Harmonize alimtaka kuachia ngoma baada ya ngoma kwani wamebaki wachache na kufanya kazi na timu ndogo ni rahisi kuliko awali wakiwa wengi.

“CHINGA ???? Tumebaki Wachache Baba Ngoma JUU Ya Ngoma,” Harmonize alimwaambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live