Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amshukuru Kajala kwa kumbadilisha tabia na kumpeleka kanisani

Harmonize Kajala Ms Harmonize amshukuru Kajala

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wanajiuliza iwapo kigezo cha dini au utofauti wa Imani katika Mungu ni suala kubwa katika ndoa na mahusiano. Ukweli ni kwamba, swali kubwa sana tena lenye mjadala pevu pindi linapoibuliwa baadhi wakisaili kama ni sahihi kwa mtu kuoa kutoka dini nyingine, kwa mfano Muislam kuoa Mkristo.

Na ndilo swali liliibuka baada ya msanii Harmonize kumvisha pete muigizaji mkongwe Fridah Kajala Masanja miezi michache iliyopita. Ikumbukwe Kajal ani Mkristo na Harmonize ni Muislam kinda kindaki.

Kila mtu anajua kwamba baada ya wachumba kuvishana pete za uchumba, hatua inayofuata ni ndoa. Watu waliibua ugumu kuhususutayarifu wa Harmonize au Kajala mmoja wao kubadili dini ili kukubali kuingia katika ndoa na mwenzake.

Lakini Harmonize katika moja ya mahojiano pindi baada ya hafla hiyo iliyofanyika Milimani City, alisema kwamba yeye hangeenda kumshrutisha Kajala kubadili dini ili kuingia katika ndoa naye.

Kweli. Kajala ndiye sasa ameonekana kumbadili Harmonize kutoka Uislam Kwenda Ukristo. Hii ni baada ya Kajala kupakia picha Jumapili wakiwa na Harmonize katika mavazi rasmi kabisa kuonesha kwamba walikuwa wanatoka sehemu kama kaanisani vile.

Kajala kwenye instastories zake, alipakia video wakicheza wimbo na Harmonize na kufuatisha kwa maneno kwamba hiyo ilikuwa baada ya kutoka kanisani. “Baada ya kutoka kanisani mimi na kijana wangu,” Kajala Masanja aliandika kwenye video hiyo ya Instastory.

Katika picha hizo, Harmonize alishukuru Kajala kwa kumgeuza kutoka kuwa kijana mtoro hadi kuwa kijana mzuri. “Mashallah mtoto wa kisukuma, ahsante kwa kumfanya kijana mtoro kung’aa tena,” Harmonize alisema.

Kajala amabye ni meneja wa kazi za muziki za Harmonize anajivunia kuwa na msanii kama huyo kuwa mchumba wake ambapo aliandika kuwa ukishampata mtu mzuri katika maisha yako basi hakuna kingine ambacho utataka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live