Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize ampa mashavu Dulla Makabila

Harmonize Ampa Mashavu Dulla Makabila Harmonize ampa mashavu Dulla Makabila

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa singeli Dulla Makabila ametoa shukurani kwa msanii wa Bongo Fleva Harmonize baada ya Konde kueleza kuwa wimbo wa singeli kuwa hit Tanzania ni wa Dulla.

Harmonize kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari nchini ameeleza kuwa wimbo ambao uliwahi kuwa hit ni ‘Pita huku’ wa Dulla Makabila, jambo ambalo lilimpa nguvu Makabila na kutoa shukurani zake kwa msanii huyo. Dulla ameandika;

“Kwanza pongezi kwa tuzo zako ambazo zimeiletea heshima nchi yetu. Pili nashukuru kwa kutambua kazi yangu japo wengi wanafahamu umuhimu wa wimbo wa ‘Pita huku’. Siyo kila mtu anaweza kuheshimu hilo, asante sana kaka. Hii imenipa nguvu zaidi ya kuendelea kupeperusha bendera ya waimbaji”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live