Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Harmonize amnunulia Kajala Range

IMG 20220413 WA0037 1140x640 Harmonize amnunulia Kajala Range

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: dar24.com

Harmonize ameendelea kuonesha hisia zake za kimapenzi na kutokata tamaa ya kutaka kurudiana na ‘X’ wake Kajala kwa kutumia mbinu za zawadi za gharama.

Licha ya Kajala kuendelea kukaa kimya na kuonyesha dalili za wazi kuwa hayuko radhi kurudiana na msanii huyo, leo hii Harmonize ameonesha gari aina ya Range Rover yenye namba za usajili kwa jina la ‘Kajala’.

Mapema jana Aprili 13, 2022, Harmonize ameonesha kipande kidogo cha video kwenye ukurasa wake wa mtandao wa instagram kikilionyesha gari hilo ambalo kwa mujibu wa maelezo yake ni kuwa ameamua kumnunulia Kajala kama zawadi ya kuombea msamaha na kuandika maneno yenye kuelezea hisia zake.

“Haziwezi kufuta maumivu niliyo kusababishia wewe pamoja na familia, haziwezi badili Clchochote tulichopitia nawala haiwezi kuwa sababu ya Kunirudia ila hiii (1) Inaeleza majuto ya yote niliyo Kufanyia, aliandika Harmonize na kuongeza,

Ninachoomba Kwako ni Msamaha wa dhati ya moyo wako  FRIDA wewe ni mtu wa Mungu Sanaa, unasali pia bila shaka Unatambua hakuna Mkamilifu hutokuja Kuanza upya Mama You Know me Better COME BACK Usisahau mimi ni mtoto wa masikini mwenzio tuu nina familia, wajomba shangazi wadogo na ndugu kibao masikini ambao nikifa Leo ndio watakao nizika Ila Nimeona Wewe Ndo unastahili hiki kidogo changu .

Katika ujumbe huo Harmonize alitamatisha kwa kusema “Natamani ujue kwamba nakupenda sana narudia teena nisamehe na unipatie nafasi ya mwisho I LOVE YOU, TAKE ME BACK nakumbuka Kuna Siku Ulishawahi niambia hii ni MOJA YA GARI YA NDOTO YAKO PLEASE TAKE IT FROM ME I LOVE YOU.” Ameandika Harmonize.

Chanzo: dar24.com