Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize amjengea ghorofa mama yake

Harmo Mama Harmonize amjengea ghorofa mama yake

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Konge Gang, Msanii Rajab Abdulkahari a.k.a Harmonize ameonesha mjengo wa ghorofa ambao anamjengea mama yake mzazi aitwaye Habiba Chivalavala.

Harmonize ameanika mjengo huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambao bado haujakamilika.

Harmonize ameambatanisha Video ya mjengo huo na ujumbe huu hapa; "Leo sijalewa nimefanya mambo ya msingi sana, hongera mama Konde sinywi tena mpaka nikumalizie kinyumba chako.

"Ya dunia ni mengi na walimwengu nao wanaomba Mungu. Muda mwingine nawaza mambo yakikaa vibaya nahamia kwako Mama Konde, sijalewa na sitolewa tena," amesema Harmonize.

Jana Agosti 15, 2023 Harmonize alitangaza kuacha pombe ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka afunguke sekeseke lililopelekea kuachana na aliyekuwa mchumba wake Kajala Masanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live