Wikendi iliyopita, staa wa Bongo alikuwa nchini Kenya ambako alitumbuiza katika tamasha lililofanyika mjini Eldoret.
Harmonize alilakiwa nchini na mtangazaji maarufu Maina Kageni ambaye alienda kumchukua Tanzania kwa ndege binafsi.
Akiwa Kenya, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alipata fursa ya kukutana na mamia ya mashabiki wake Wakenya pamoja na watu wengine maarufu. Miongoni mwa watu maarufu aliokutana nao ni mwimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili Christina Shusho ambaye alikiri kuwa ni mwanamuziki wake kipenzi.
""Nimekutana na mwimbaji ninayempenda, OMG, Nampenda Christina Shusho. Nakufa kwa sauti yake," Harmonize alisema chini ya video ya mkutano huo wake na Shusho ambaye kwenye Instagram.
Katika video hiyo, staa huyo wa Bongo alionekana akimkumbatia Shusho kabla ya kupiga goti na kubusu miguu yake.
Shusho alionekana akijaribu kumwinua mwanamuziki huyo mwenzake wa Tanzania kabla ya wote wawili kufurahia mazungumzo mazuri.