Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize akiri kupewa somo na Kanumba

Jharmo Kanumba Kl Harmonize akiri kupewa somo na Kanumba

Sat, 27 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Fleva, Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram, amekiri kuwa alipata mafunzo mengi ya kimaisha kutoka kwa filamu za aliekuwa Mfalme wa Bongo Movies, marehemu Steven Charles Kanumba.

Konde Boy alisema ingawa hakupata nafasi ya kukutana na Kanumba, lakini alijifunza unyenyekevu kwa kumtazama kwenye runinga wakati akiwa hai na hata baada ya kifo chake.

"Kanumba made me to be so humble ingawa sijawahi hata kumuona mpaka anatangulia kifupi hanijuwi," Harmonize aliandika.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alimtakia Kanumba mapumziko ya amani huku miaka 10 ikiwa imepita tayari tangu kifo chake.

Muigizaji huyo alifariki mnamo Aprili 7, 2012 kutokana na jeraha la kichwa baada ya kuanguka katika chumba chake cha kulala.

Wakati wa kifo chake, Kanumba alikuwa pamoja na aliyekuwa mpenziwe na pia muigizaji mwenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye baadae alishitakiwa kwa kosa la mauaji bila kukusia kisha kufungwa jela na alipomaliza adhabu yake aliachiwa huru.

Takriban miezi mitano iliyopita mamake Kanumba, Flora Mutegoa alitoa shukrani kubwa kwa bosi wa WCB, Diamond Platnumz kwa kumkumbuka marehemu mwanawe kwenye wimbo wake 'Nawaza'.

Mjane huyo alisema aliridhishwa na kitendo cha Diamond kumsherehekea mwanawe hasa katika kipindi hicho kilichokuwa cha kumbukumbu ya kifo chake.

"Ameweza kumkumbuka marehemu Steven Charles Kanumba. Haikuwa rahisi. Nilipousikia nilifarijika, nilifurahi sana, kumbe bado anamkumbuka! Mwezi ujao, tarehe saba tunamaliza miaka kumi," alisema mama Kanumba.

Mama Kanumba alisema ni jambo la maana kuona Diamond akimuwaza mwanawe kwani ni wengi ambao tayari wamemsahau mwigizaji huyo aliyeshabikiwa kote duniani.

Katika wimbo wake 'Nawaza', Diamond katika moja ya mashairi yake ameimba; "Huenda Kanumba angelikuwepo hai, Nawaza movie zetu pia tungejidai."

Muigizaji Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Kanumba huwa anaadhimisha kifo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live