Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize akata tamaa ya kupenda tena

Harmonize Harmotz Harmonize akata tamaa ya kupenda tena

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Suala la kuingia kwenye Mahusiano tena limekuwa mtihani sana kwa mwanamuziki Harmonize ni kama vile amekata tamaa na mahusiano.

Kupitia Instastory yake Harmonize ameweka wazi kuwa kwa sasa hana hisia za kupenda tena licha ya kutokea wasichana wengi wanaotamani kuwa naye kwenye mahusiano.

Harmonize ameandika;

"Wanawake wengi wazuri wamejitahidi kunishawishi kupenda tena kwa sababu wanajua ninapopenda nakuwa rafiki, mume, mtoaji na baba bora, nalikubali hilo. Lakini moyo wangu kwa sasa hauko tayari kupenda kabisa. Natumaini sitokuwa hivi daima. Niombeeni ili moyo wangu uweze kuruhusu kupenda tena."

Harmonize amefikia hatua hiyo baada ya kuachana na Kajala Masanja kwa mara ya kwanza kisha kurudiana naye na sasa wameachana tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live