Menu ›
Burudani
Wed, 23 Aug 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul 'Harmonize' amesema kwa sasa yupo singo na amekaa siku 30 bila kumjua mwanamke.
Mwamba ametoa kauli hiyo kupitia Insta Story yake ambapo amesema, alikuwa na mahusiano ya mbali lakini hata hivyo kwa sasa yupo singo na mwanamke atakayemtangaza kuwa naye ndiye atakayemuoa.
"Mwanamke atakayekuja Konde Village ukiondoka ndugu zangu basi atakuwa ni mfanyabiashara au rafiki yangu tena wa karibu," aliandika Harmonize.
"Nimerudi mtaani na nitakuw bize na muziki, sitataka mtu aniulize kuhusu mambo yasiyohusu muziki," alimalizia Harmonize.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live