Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize aiteka ngome ya Diamond

DIAMOND HARMONIZE ASD Harmonize aiteka ngome ya Diamond

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize au Konde Boy; yeye anasema kuwa ndiye msanii namba moja kwa sasa nchini Tanzania baada ya kufanya shoo ya kibabe na kujaza ukumbi mkoani Kigoma wikiendi iliyopita.

Harmonize ametamba kuiteka ngome (base) hiyo ya Kigoma ambayo inafahamika ni ngome ya mwenyeji Diamond Platnumz na wakati f’lani pia ni ngome ya King Kiba.

Kigoma unaweza kusema ni nyumbani kabisa kwa Diamond kwa sababu asili yake kwa upande wa mama yake, Mama Dangote ni mwenyeji wa Kigoma; sehemu ambayo Diamond alishakiri kwamba ni ngome yake na ndiyo maana alikwenda kuadhimisha miaka 10 ya muziki wake, lakini sasa mambo yamebadilika.

Harmonize ambaye ngome yake kuu ni Mtwara amefanikiwa kukusanya mashabiki wengi kuanzia alipotoa kwenye uwanja wa ndege ambapo alilakiwa na rundo la bodaboda kisha watu kuzingira hoteli aliyofikia na mwisho kuimba naye nyimbo zake zote wakiwa ukumbini huku Polisi wakifanya kazi kubwa kutuliza vurugu kutokana na wingi wa watu.

Akishukuru kwa umauti huo kujitokeza na kuonesha mapenzi makubwa kwake, Harmonize alirusha kijembe kuwa hata Kigoma ni ngome yake kwani ndiye msanii namba moja Tanzania.

Hata hivyo, wakati Harmonize akitoa tambo hizo, kwingineko huku Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Diamond aliangusha bonge la shoo iliyokwenda kwa jina la VIP Show ya ukumbini kisha shoo nyingine uwanjani.

Kwa mujibu wa video mbalimbali za runinga za mtandaoni nchini humo, shoo za Diamond zimeweka rekodi kwa kujaza na viingilio vikubwa ambavyo hata wasanii wenyeji nchini humo hawatozi viingilio vikubwa kiasi hicho.

Kiingilio cha chini kabisa kwa mujibu wa mabango kilikuwa ni Dola za Kimarekani 50 ambazo ni zaidi ya shilingi laki 110 za Kitanzania kwa mtu mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live