Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize afunguka sababu ya kuonyesha maisha yake ya kifahari

Harmonize(1) Harmonize afunguka sababu ya kuonyesha maisha yake ya kifahari

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Rajab Abdulkahari a.k.a Harmonize amedai kuwa akionesha maisha ya kifahari anayoishi hamaanishi kuwa anawatambia watu bali anawatia moyo kwenye utafutaji.

Harmonize amesema hayo wakati akiwakumbusha mashabiki wake ujuo wa ngoma yake mpya ya Single Again Remix anayotarajia kuachia hivi karibuni ambayo amemshirikisha staa wa Afrobeats kutoka Nigeria, Michael Adebayo Olayinka 'Ruger'.

Kupitia #Instalive video ambayo ameingia jana msanii huyo hakusita kuonesha mjengo anaoishi, na sehemu za kujivinjari zilizopo katika nyumba hiyo, huku akidai kuwa pamoja ya kuwa na sweaming pool ndani lakini hajaitumia kwa miezi sita.

Harmonize amewataka watu kutokata tamaa kwenye utafutaji kwani hata yeye hakutegemea kama atakuja kuishi maisha anayoishi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live