Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize afunguka "Mama alinitahadharisha kumuoa Kajala"

Kajala Na Harmonize Mjadala Harmonize na Kajala

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amedokeza kuwa mama yake alimtahadharisha kuhusu aliyekuwa mpenzi wake.

Katika ufichuzi ambao alifanya kama ushauri, bosi huyo wa Konde Music Worldwide  aliwashauri watu kuwapa sikio wazazi wao kila siku. Harmonize  alibainisha kwamba wazazi huwa na jicho maalum la kuwasaidia kuona mambo yaliyofichwa ndani ya mtu.

"Msikilize mama!! Awe ni mama yako mzazi au mama wa mwenzio, baba yako ama wa mwenzio.. wazazi wanakuwanga na jicho la mbali sana. Mzazi ni rahisi kugundua kila kitu.

"Inawezekana ukawa unajiona unajua kila kitu kumbe kuna jicho la mama. Akiangalia kitu au mtu anapata jibu sahihi kuliko wewe," alisema siku ya Alhamisi.

Mwimbaji huyo mahiri aliwasihi watu kutilia maanani pingamizi zinazowekwa na wazazi wao bila kujali jinsi zinavyochukiza. Pia, aliwataka watu kuwasikiliza wazazi wa wenzao hasa kuhusu masuala ya uhusiano bila kujali jinsi mahaba yalivyo mazito.

"Unaweza kuona kama kwamba huyu mama hanipendi akiwa mama wa mwenzio kumbe  huenda anajua kwamba mtoto wake hayupo tayari ila anakosa au anashindwa jinsi ya kukufanya uelewe maana upo kwenye dimbwi la mapenzi," alisema.

"Akiwa mzazi wako ni rahisi kukukataza hata kwa kutumia nguvu zote ila ukiwa umezama humuelewi," 

Wakati huo, alifichua kwamba hapo awali karibu aingie kwenye ndoa mbaya ambayo mzazi wake alikuwa amemuonya dhidi yake.

"Mtu anayeitwa mzazi msikilize hata asiyekuwa wako," alisema.

Staa huyo wa Bongo alitangaza kwamba atafanya ufichuzi zaidi kuhusu kilichofanyika mnamo siku ya wapendanao, Februari 14.

Pia alisisitiza kwamba kwa sasa hayuko kwenye mahusiano yoyote huku akionyesha kujivunia kwake kuwa single.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live