Mwendelezo wa sakata la Harmonize, Kajala na Paula. Baada ya Kajala na Paula kuzungumza kupitia kipindi chao, Harmonize ameibuka na kuwachamba mambo mbalimbali.
Miongoni mwa hayo mambo ni kufichua siri ya kumnunulia pizza na mawigi Paula na anashangaa kwa nini anamkana, hakumbuki fadhila hizo.
"Aaah Dapauu! Hata mawigi na Pizza alizokuletea Boda Kimara kwa Bibi Wweek before muende Moshi mkashawishiana huko mnirekodi nazo unazikataa!! Alafu (halafu) unajitoa mapema sana kwenye hii vita binti yanguu wakati we ndio mpambe!! Utanizalilisha (utanidhalilisha) mara ngapi mie kushinda video! Una nyingine achia tuondoke maana sidhani kama tuliongea mara moja! Mnyookee bi mkubwa atulie muda umeisha,” aliandika kwenye Insta Story Harmonize.