Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul 'Harmonize' amesema lengo la yeye kujiita Bakhresa lilikuw ni kujitia moyo wa kimafanikio kama aliyonayo mfanyabishara Said Bakhresa.
Hamonize amesema, hakujiita hivyo ili pengine labda waweze kukutana lakini ikitokeoa pia hawezi kukataa kwani ni mtu anayemkubali katika watu ambao wamefanikiwa na hawana makuu.
"Imenipa funzo kwamba hata mimi nikijiangalia na vihela vyangu natamani nijioneshe nini lakini nikimuangalia yeye naona mbona hana hizo mambo hivyo unapata fundisho kubwa la maisha," alisema Harmonize alipokuw akihojiwa na Clouds FM nyumbani kwake Salasala jijini Dar.