Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize adaiwa kumtumia Kajala na Paula kumuumiza Rayvanny

Harmonize Kajala Mc Harmonize adaiwa kumtumia Kajala na Paula kumuumiza Rayvanny

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize; ni msanii mkubwa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye kwa sasa amekuwa karibu mno na mchumba’ke, Kajala Masanja na bintiye Paula Kajala.

Sasa; inasemekana kwamba kitendo hicho kinamuumiza mno ex wa Paula ambaye ni Rayvanny.

Hii ni kufuatia Rayvanny kutokuwa na uelewano mzuri na Harmonize ambaye ni memba mwenzake wa zamani katika Lebo ya WCB ya Diamond Platnumz.

Inafahamika kwamba, baada ya Harmonize kurudiana na Kajala, kwa upande mwingine Paula alitengana na Rayvanny ambapo jamaa huyo alirejea kwa baby mama wake, Fahyma.

Baada ya Harmonize kumvisha Kajala pete ya uchumba, Paula alithibitisha ule usemi kwamba mtoto hakui kwa mzazi wake na hakuna mkate mgumu mbele ya kikombe cha chai ya rangi na wenye midomo wanasema aliyemuoa mama ndiye baba.

Paula sasa anamkubali Harmonize kama baba’ke na ameonekana kuufurahia uhusiano wake na mama’ke hadi katika muziki ambao Kajala ndiye meneja wa kazi za muziki za Harmonize.

Paula amekuwa amekuwa akimsifia Harmonize na kurusha vijembe kwa wapinzani wake akiwemo Rayvanny akisema kuwa anajua muziki hadi anajua tena na hakuna wa kumfananisha na Jeshi; jina ambalo linatumiwa pia na Harmonize.

“Ninyi wote hamko tayari kwa dude jipya? Baba unajua mpaka unajua tena Harmonize,” Paula aliandika kwenye insta story yake, kuonesha kwamba amemkubali Harmonize kama baba.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanasema kuwa, Rayvanny atulie kwa mama mtoto wake, Fahyma kwani wametoka mbali na akumbuke kutesa ni kwa zamu, maana kuna kipindi WCB nzima na machawa wao walimtumia Paula kumuumiza Harmonize hivyo naye avumilie dawa imuingie.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live