Drama zimepamba moto huku malkia wa WCB, Zuhura Othman almaarufu Zuchu na mpenzi wa Harmonize, Poshy Queen wakirushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.
Drama ilianza baada ya Konde Boy kumkejeli Zuchu muda mfupi baada ya kutoa taarifa kueleza kwa nini alijiondoa kwenye uhusiano wake na Diamond Platnumz.
Bosi huyo wa Konde Music Worldwide aliposti video ambayo ilionekana kumshambulia moja kwa moja Zuchu na alionekana kumcheka kutokana na matatizo katika uhusiano wake.
“Kibonge koma @harmonize_tz Huna hit mjini una kazi ya kuchambana tu hujui nini sijui eeh nioneshe,” Zuchu alimwandikia Harmonize kupitia mtandao wa Instagram.
Aliongeza; “Harmonize baba zima kazi ya kudandia visivyokuhusu. Mwanamke wako yuko busy kuomba nafasi kwa huyo unayejifanya nusu yako shenzi. Koma kistuli.”
Kufuatia kushambuliwa kwa mpenzi wake, Poshy Queen alizamia kwenye akaunti yake ya Instagram na kumshambulia Zuchu akimkejeli kuhusu mwili wake mdogo. “Sisi koma. Mwili mzima kucha hadi nywele kalio langu la kushoto!! Muulize tena!! Shem kama shem nimeingiaje humu,” Poshy Queen aliandika.
Harmonize naye alionekana kuendelea kumkejeli Zuchu kwenye akaunti yake ya Instagram kupitia video za kejeli na kauli ambazo ali-share.
Haya yanajiri katika kipindi ambacho Zuchu na Diamond wameripotiwa kuachana tena.
Kulikuwa na tetesi kuwa binti huyo wa malkia wa Taarab, Khadija Kopa amemuacha Simba, ambaye pia ni bosi wake baada ya kumtambulisha ex wake, Sarah katika tamasha la muziki la hivi majuzi.
Wakati wa tamasha hilo, Diamond alimwita Sarah jukwaani na kufunguka jinsi alivyomshawishi kuandika wimbo wa ‘Kamwambie.’
Zuchu hata hivyo, alikanusha madai ya kuachana na bosi huyo wa WCB kwa sababu ya Sarah na badala yake akaeleza kuwa mpenzi wake ndiye aliyemfanya akosewe heshima na watu.