Mwanamuziki Harmonize ametoa kile kilichopo ndani ya moyo wake juu ya mwenendo wa wasanii wa muziki wa Bongofleva kutokuwa na ushirikiano hasa kupeana support ili kukuza muziki wa Bongofleva Kimataifa.
Bosi huyo wa Konde Gang ameeleza kuwa, moja ya kitu kinachopelekea muziki wetu kutokuwa mkubwa ni chuki zisizo na maana miongoni mwa wasanii.
"Tunasikilizwa Afrika Mashariki pekee, ndipo tunapoelewaka," ameeleza Harmonize kwenye sehemu ya ujumbe wake kupitia insta story.
Pia, Harmo ametolea mfano wanamuziki wa Nigeria akisema wanawachora tu wasanii wa Bongo walivyokuwa hawapendani, wao wako busy ndio maana hawagombani. Wasanii wa Bongofleva wanapishana humu humu ndio maana wanarushiana maneno.
Amebainisha kwamba chuki zitaisha ama kupungua ikiwa msanii una stress za kuujaza O2 Arena (London) siku 3.
"Kiuhalisia tunapendana sana. Sisi ni familia moja, DJ's, wadau, mashabiki na wasanii," amemalizia Harmonize kwenye ujumbe wake.