Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Siwezi ona kipaji cha Anjela kikiteketea

F06d670662047a9aad4cbae345f4c67b Harmonize: Siwezi ona kipaji cha Anjela kikiteketea

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amesema atamsaidia Anjela kwa namna yeyote licha ya kuwa na ulemavu na amemshirikisha kwenye wimbo wake wa kwanza kabisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alichapisha picha ya Anjela na kuandika maneno haya:

“Niliuambia moyo wangu kwamba siwezi ona kipaji cha huyu dada kinateketea eti kwa sababu tu ana ulemavu, ambao amebarikiwa na Mungu ambaye kazi yake haina makosa na hajawahi kukosea,”.

“Hakuna mwenye haki ya kuikosoa iwe kwenye jua mvua nitahakikisha kipaji chake kinawafikia mtaamua ninyi kumuunga mkono au laa. Nimemshirikisha kwenye wimbo wangu wa kwanza kabisa mwaka 2021,”

Alisema ana imani amemfungulia milango mingi na kuifikia ndoto yake alioikimbilia kiujasiri na kujiamini bila kujali mapungufu ama ulemavu aliotunukiwa na Mungu uenda ingekuwa sababu ya kukata tamaa na ukizingatia ni mtoto wa kike

Baada ya Harmonize kuchapisha maneno hayo Anjela aliandika ujumbe huu.

“Eeeh Mungu nakushukuru kwa kunikutanisha na Harmonize kupitia yeye nimeheshimika kwa kweli nina furaha ambayo sikuwahi kuipata maisha yangu yalikuwa ya kutengwa tu kutokana na ulemavu niliokuwa nao amani na furaha niliyokuwa nayo sasa siwezi kuelezea, nakushukuru Mungu nakushukuru,”

Chanzo: habarileo.co.tz