Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Siwezi kubishana na Mkubwa Fella

Harmonize X Diamond Harmonize: Siwezi kubishana na Mkubwa Fella

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CEO wa Konde Gang Music Harmonize anasema hawezi kumjibu chochote meneja wa WCB, Yamoto Band na TMK Wanaume Family Mkubwa Fella baada ya kusema kuungana kwa Harmonize na Rayvanny bado hawamuwezi Diamond Platnumz.

“Kupata na Rayvanny lengo letu sio kumshusha msanii yeyote, kwanza Mkubwa mimi namheshimu sana. Kwa bahati mbaya sijawahi kupitia kwake. Ni kitu cha kujivunia kwamba pengine ningepitia Mkubwa na Wanawe ningekuwa ningepita exposure zaidi kwa sababu kile ni kama chuo cha muziki ambacho wamepitia wasanii wengi sana, lakini bahati mbaya mimi sikupita.

“Mimi namuita Mkubwa Fella Baba, kwa vitu ambavyo amevifanya kwenye industry ya muziki hapa nchini mimi hata angezungumza nini nisingeweza kusema chochote kwa sababu mimi bado ni mdogo sana kwenye muziki, hata akisema nini mimi nitasema tu ndio, ndiyo, ndiyo mkubwa yaishe.

“Sisi ni watu wazima tunakuwa, rayvanny is my brother, tunapishana kidogo kiumri yawezekana nikawa namzidi kidogo tu, tukiwa na matatizo kwenye umri huu na tukaamua kuyamaliza, ilitakiwa Mkubwa awe proud aone kwamba vijana wanakuwa wala sio kuingiza ushindani. Mkubwa ni mzazi wangu kama wazazi wengine, nitaendelea kumheshimu tu," amesema Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live