Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Sitembei na wafanyakazi

Harmonizee Zuu Harmonize: Sitembei na wafanyakazi

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize au Konde Boy Mjeshi; ni staa mwingine mkubwa wa muziki nchini Tanzania ambaye baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Bakhresa ameeleza sifa za Bakhresa ambaye ni tajiri mkubwa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Harmonize, miongoni mwa sifa za Bakhresa ni mtu ambaye hana tabia ya kutembea na wafanyakazi wake.

Anasema; “Sifa ya Bakhresa ni mchapakazi…!!! Hachagui biashara hadi tui la nazi…!!! Anaamini mafanikio ni hatua kama kupanda ngazi…!!! “Bakhresa hana hulka ya kutembea na wafanyakazi…!!! Matajiri hawana time kuongea…!!! Lini ulishasikia Bakhresa anazungumza umbeya…”

Kauli hiyo ya Harmonize juu ya Bakhresa kutotembea na wafanyakazi wake inasemekana ni kijembe kwa bosi wa zamani wa Konde Boy ambaye ni Diamond Platnumz ambaye kuna tetesi kuwa anatoka na msanii wake, Zuchu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live