Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Sitaenda shoo ya msanii mwenzangu bila kulipa tiketi

Harmonize Mla Harmonize

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Fleva Tanzania Harmonize ameandika maelezo kuhusu wazo lake la kufanya shoo na kulipisha kila kichwa bila Mialiko, Harmo anasema....

Harmonize Ameandika;

"Wazo Lilianza Nilipo Ona Kuwa Sisi Tuliopo Kwenye Industry Uwongo Dhambi Hali Zetu Sio Mbaya Sana Ila Tukiandaa Show Imekuwa Kawaida Kuitana Kualikana Bure Bure Tunapoenda Viwanjani Kwa Watu Ambao Ni Wazi Kabisa Tunawazidi Kipato Kwa kuwa Tu Wanatupenda.

Basi Tunatumia Hizi Nafasi Kuwakamua Walipe Hela Kutuona Wakati Wenyewe Kwa Wenyewe Hatu Changiani Haliyakuwa Uwezo Wakulipa Tunao.

Nitoe Tu Shukrani Kwa Wasani Wenzangu Wote Mliolipokea Hili Wazo Na Mkanunua Meza Kwa ajili Ya Shoo Yangu Kesho.

Hakika Nyinyi Ni Mfano Wa Kuigwa Kwa Maendeleo Ya Tasnia Hill !iii Niwaahido Tuu Sitoenda Kwenye Show Ya Msani Mwenzangu Yeyote Bila Kununua Tickets Au Meza Naamini Ni Njia Sahihi Ya Kufungua Mlango Mwingine Wa Ridhiki Leo Na Vizazi Vijavyo Tupo Wengi Sanaa Tunapata Ridhiki Alhamdulilah Tukutane Kesho"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live