Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize, Sallam SK wamaliza bifu lao kiume

Screenshot 20221212 075536 Instagram Harmonize, Sallam SK wamaliza bifu lao kiume

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KWA mara ya kwanza, mwanamuziki na CEO wa Konde Ganda, Harmonize amekutana na kusalimiana na bosi wake wa zamani ambaye ni Meneja wa lebo ya WCB, Sallam SK visiwani Zanzibar.

Harmonize ambaye yuko visiwani humo kwa ajili ya shoo yake, amekutana na Sallam ambaye walikuwa na ugomvi mkubwa ambao uliibuka baada ya Harmonize kujitoa WCB na mara kadhaa wawili hao walifanya mahojiano na kila mmoja kuzungumza mabaya ya mwenzake ambayo alimfanyia.

Tukio lililoibua gumzo na kuthibitisha kwamba wawili hao wana vita, ni pale ambapo Sallam SK alipokataa mkono wa salamu wa Harmonize kwenye msiba wa mke wa Babu Tale mkoani Morogoro mnamo Juni mwaka 2020, na baada ya hapo yaliibuka maneno mengi.

Video inayosambaa mitandaoni inaonesha kwamba wawili hawa wamemaliza tofauti zao na kwa sasa wana maelewano mazuri ndio maana kwenye video Harmonize amemwambia Sallam kwamba anampenda sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live