Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize, Rayvanny kimenuka! Watifuana kinoma

Harmonize Na Rayvanny Watifuata Harmonize, Rayvanny kimenuka! Watifuana kinoma

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ulimwengu wa burudani tangu jana, umepambwa na mtifuano wa kurushiana maneno kati ya mastaa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul 'Harmonize' na Raymond Mwakyusa 'Rayvanny'.

Ishu ilianza baada ya Harmonize kuandika kwenye Insta Story yake kwamba wasanii waache kuimba nyimbo za pombe.

"Wasanii punguzeni nyimbo za pombe msidhani hii nchi kila mtu ni mlevi! Hata tunaokunywa Jumatatu hatunywi tukizisikia nyimbo za pombe kama unatonesha kidonda hasa hii Januari."



Hapo ndipo alipomuibua Chui ambaye alishuka na gazeti refu hatari ambapo alianza kwa kuandika hivi:

"Huna ngoma ya pombe iliyowahi kuhit sasa utaongea nini kuhusu mawe ya pombe shut the... (tusi) Nitongoze video soon."



Kama hiyo haitoshi, Rayvanny alizidi kutiririka kuwa, nyimbo za pombe ni nzuri na zinapendwa na kujitapa kuwa wakati yeye anaandika nyimbo za pombe, Harmonize alikuwa bado hajaanza muziki alikuwa akiuza mitumba.

Rayvanny alizidi kutema shit kuwa, hata wimbo wa Mandakiwe haukuwa wake na kwamba alilipa shilingi milioni 600 akalia kwenye vyombo vya habari wakati ni jambo la kawaida kulinganisha na yeye ambaye alipotoka Wasafi, alilipa Shilingi Bilioni 1.3.

Rayvanny alienda mbali zaidi kwa kusema, kama haamini, aende BASATA akaulize kuhusu kiasi hicho cha pesa alicholipa na ataambiwa ukweli.

Chui aliendelea kwamba, hata wimbo wa Paranawe aliandika yeye na kwamba hata zile video za utupu za Harmonize hakuvujisha yeye na kumtaka awaangalie watu wanaomzunguka ndio waliovujisha.

Rayvanny alijitapa kwamba yupo vizuri kifedha kuliko Harmonize. Harmonize alirudi tena baadaye na kumtaka aimbe muziki wa Piano na waache kuimba nyimbo za pombe.

Harmonize alisema, Rayvanny alivujisha picha za utupu ili pengine ajiue lakini haikuwa hivyo, yupo na pengine Mungu alitaka awe hai ili aweze kujifunza kutoka kwake.

Meseji hizo zimetapakaa mitandao mbalimbali na kila mtu kutoa maoni yake. Wapo wanaokubaliana na Harmonize, wengine wanamkubali Rayvanny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live