Ikiwa ni siku moja baada ya aliyekuwa mchumba wa msanii Harmonize aitwaye Sarah Michelotti kuibukia mahakamani na kudai mali zake alizochuma na msanii huyo, mapya yameibuka tena.
Kupitia Insta stori yake, msanii Harmonize ame-share chats zake na mchumba wake wa sasa Kajala Masanja akidai kuwa alikosa mahali pa kulala baada ya kuachana na Sarah.
Sarah alifika mahakama maalum inayoshughulikia kesi za talaka, mirathi na watoto wilaya ya Temeke, Dar es Salaam jana Septemba 27, 2022 ikiwa ni muendelezo wa madai ya talaka kati yake na Harmonize.
Pia, inadaiwa kuwa Sarah anataka talaka na mgawanyo wa baadhi ya mali ambazo bado zipo kwa Harmonize.
Ikumbukwe kuna muda Harmonize alihojiwa akasema walishamalizana na Sarah, lakini mrembo huyo aliibuka kusema sio kweli kuna mambo Harmonize anadanganya.
Aidha, ikumbukwe pia kuwa, Harmonize na Sarah walifunga ndoa mnamo Septemba 7, 2019 na kufanya sherehe kubwa Masaki jijini Dar es Salaam iliyohudhuriwa na mastaa na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa muziki.