Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Harmonize ameasema kuwa aliyekuwa mpenzi wake, Kajala Masanja alifika hatua akaiba kadi ya gari alilokuwa amemnunulia kabla ya kuachana.
Harmonize mesema hayo kupitia InstaStory yake na kudai kwamba Kajala alichukua kadi ya gari yake aina ya Range Rover lakini kwa sababu aliamini wamekuwa kitu kimoja hivyo alikuwa hafichi vitu vyake mfano kadi ya gari.
CEO huyo wa Konde Gang amedai kuwa kuna siku ameamka na kwenda sehemu zinapokaa kadi za gari hakuna kadi ya gari moja akauliza kadi ilipo lakini hakupata jibu hivyo akajua kabisa kwamba huenda mwenzake tayari alikuwa akijianda na maisha mengine nje ya mahusiano yao.
"Maskini ya Mungu tunalala wote tunaamka tunafanya hili na lile, ninamiliki gari zaidi ya 10 halafu mwenzangu hana hata 1. Sisi ni binadam kesho yetu ipo mikononi mwa Mungu ikitokea leo sipo Mama Konde & Zuuh Konde wataondoka na kila kitu, hawatomuelewa dada wa watu acha hii gari ya ndoto yake nimfanye kuwa mmiliki halali, kosaaaa!.
"Unakuta mnapowekaga kadi za magari, kadi 1 haipo imeenda wapiii nitatafuta kiutuuzima unajiongeza tuuu, kuwa mwenzetu anajiandaa na maaisha mengine kikubwa uhai kama.
"Pesa zinatafutwa kunakoelekea atanitoa roho huyuu kama bado unahisi sija #Moveon ni tatizo lako la uzeeee piaa. Sikukugombeza sikukutukana nilikudharau na ndio maana umekuwa ukisema akimzoea mtu anamdharau.
"Hakuna aliekuwa anajua hili hata watu wa karibu ndiomaana kila mtuu alikuwa anadhani labda nime chiiiiiit na sijuwi amelowa girl lol nadhani level ya mwanamke wangu unaijua Humgiki hata robo, mwizi mtuuu mzimaaaa," amesema Harmonize.