Leo Julai 22, ni kumbukizi ya mfanano wa siku ya kuzaliwa ya Kajala Masanja ambapo mchumba’ke, Harmonize amemtakia kila la heri kwa kusema;
“Thanks 4 changing my life baby you have made me a real sportsman. Now kile kitambi vp lol...........”
Maneno hayo ya Harmonize yanamaanisha kwamba Kajala ndiye aliyekuwa akimsisitiza kufanya mazoezi ili kuondoa kitambi.
Hilo ni kweli kwa sababu kabla ya wawili hawa kurudiana kuna picha za Harmonize zilitapakaa mitandaoni zikimuonesha akiwa na mwili wa ajabu.
Wengi walimponda Harmonize kutokana na mwili huo na taarifa hizi Harmonize alikuwa anazipata na zilimuuma ndiyo maana hata leo hii anamshukuru Kajala kwa kuchangia kumaliza kitambi chake.
Kajala ndiye ndiye chachu ya Harmonize kushinda gym akifanya mazoezi.