Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize, Kajala hawakamatiki huko

Harmonize Na Kajalaaaa Harmonize, Kajala hawakamatiki huko

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize au Konde Boy; ni msanii mkubwa muziki nchini Tanzania ambaye wikiendi iliyopita ameacha historia kwenye shoo jijini Bujumbura nchini Burundi akiwa sambamba na mchumba’ke, Kajala Masanja.

Mashabiki wa Konde Gang walifurika kwenye shoo hiyo ambayo kiingilio kilikuwa ni elfu 10 kawaida na elfu 50 VIP, lakini tiketi zote ziliisha na kuonesha ukubwa wa Harmonize kwani ilikuwa ni shoo ya mtu mmoja (one man show).

Katika shoo hiyo, Harmonize alianza kutumbuiza saa 4:00 usiku hadi saa 6:00 usiku bila kupumzika na kukata kabisa kiu ya burudani kwa mashabiki wake.

Kitu cha kipekee na ambacho mashuhuda wanathibitisha ni kwamba, mashabiki hao walikuwa wanaimba na Harmonize nyimbo zake zote kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Wenyewe mashabiki hao wanasema kuwa, shoo ya Harmonize ndiyo shoo pekee ambayo wamepata kuiona katika jiji hilo la Bujumbura katika miaka ya hivi karibuni.

Jambo lingine lililoibua shangwe kama lote ni baada ya Harmonize kumpandisha jukwaani Kajala ambaye mbali na kuwa mpenzi wake, pia ni mmoja wa mameneja wake.

Harmonize aliwahakikishia mashabiki hao kuwa, ni kweli Kajala amemsamehe na sasa ni mkewe na ni bosi wake, jambo ambalo liliwafurahisha mno mashabiki hao.

Uchunguzi unaonesha kwamba, katika shoo zote ambazo Harmonize amekwenda na Kajala nje ya Tanzania kuanzia kule Quarter, Kongo na Burundi; zote ni shoo ambazo wameacha alama ya burudani ya kukata na shoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live