Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Kajala ananitafuta anataka turudiane

Harmonize Na Kajala Harmonize: Kajala ananitafuta anataka turudiane

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Fleva, Harmonize ameeleza kuwa aliyekuwa mpenzi wake, Kajala Masanja bado anamtaka na bado anatamani warudiane.

CEO huyo wa Konde Gang ameongeza kuwa mara nyingi amekuwa akimtumia meseji za kutaka kurudiana na huenda huwa anawaza atakutana na bango la TAKE ME BACK.

Harmonize ameenda mbali zaidi na kusema kuwa Kajala alishawahi kumkatia mama yake Harmonize tiketi ili aje Dar es Salaam asuluhishe ugomvi wao.

Aidha, Harmo ameongeza kuwa mara nyingi Kajala anamtafuta meneja wa Konde Boy, Jembe ni Jembe ili amuimbee msamaha baada ya kwenda nyumbani kwa Harmonize kumuomba warudiane lakini walinzi walimfukuza.

Mastaa hao walikuwa kwenye uhusiano lakini waliachana kabla ya kurudiana tena ambapo hawakuchukua time wakapigana chini tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live