Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Hakuna Konde Boy bila Madam Rita

Madam Rita Harmonize: Hakuna Konde Boy bila Madam Rita

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize au Konde Boy Mjeshi; ni staa wa muziki nchini Tanzania akimiliki Lebo ya Konde Music ambaye amempigia magoti bosi wa Shindano la BSS, Madam Rita kama njia moja ya kutoa shukrani kwa kumsaidia kujenga kipaji chake.

Ishu hiyo imejiri katika Tamasha la Serengeti Festival lililofanyika jijini Dodoma wikiendi iliyopita huku Harmonize akionesha hisia nyingi jukwaani.

“Siyo lazima mtu akuambie yes ndiyo usaidike, anaweza akakuambia no na akawa amekusaidia. Niseme kweli, hakuna Konde Boy bila Madam Rita,” anasikika Harmonize akiwa stejini.

Kama utakumbuka, miaka ya nyuma Harmonize aliwahi kushiriki Shindano ya Bongo Star Search (BSS) ambayo Madam Rita ni Chief Judge, lakini hakufanya vizuri hata hatua ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live