Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Diamond hana uwezo wa kunilipa sh millioni 600

Harmonize Tz Tz Harmonize: Diamond hana uwezo wa kunilipa sh millioni 600

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Harmonize amejibu mapigo huku akimuonya aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz akidai kuwa, msanii huyo hana uwezo wa kumlipa Tsh milioni 600 ili waimbe pamoja.

Harmonize anasema; "Tatizo masikini huyu hukumbuka wanawe akishakusanya mali zake, Anyway haiwezi kuja kutokea, hiyo miaka 15 maana Tsh millioni 600 kunilipa hutoweza!."

Ikumbukwe mapema usiku wa kuamkia juzi Diamond alitangaza onyesho maalum la miaka 15 katika muziki, huku akitamani uwepo wa wasanii ambao amewatoa kimuziki.

Baada ya onyesho, Harmonize aliingia kwenye IG Story akidai kuwa amechoshwa kutajwa kila siku kuwa ametolewa na mmiliki huyo wa lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live