Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize Amponza Jane Misso

Harmonize Omoyo Harmonize Amponza Jane Misso

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMAMA anayeimba Nyimbo za Injili, Jane Misso amekiri kuponzwa na wimbo alioimba na staa wa Bongo Fleva, Harmonize.

Jane Misso ambaye ni Mkristo anasema kuwa, baada ya kutoa Wimbo wa Omoyo Remix akishirikiana na Harmonize ambaye ni Muislam, baadhi ya watu wamemtenga.

“Tunatofautiana sana uwelewa na siyo makanisa yote yamenitenga, kuna wengine mbona wame-support, maaskofu wengi, wachungaji wengi wamefurahia sana, wamefurahi mno.

"Kitu ambacho sikutegemea, lakini wengine wameonekana kukwazika na hata kuna wengine nilikuwa na safari zangu kuelekea sehemu f’lani wamesema wame-cancel, lakini mimi sishangai,” anasema Jane Misso.

Anasema kuwa, anawapa muda wanaohoji kwa nini ameamua kuimba na Harmonize akisema hata Yesu alijichanganya na wenye dhambi hivyo hajaona kama kuna tatizo.

Jane Misso anammwagia misifa kama yote Harmonize kwa kusema kuwa ni kijana mwelewa, mnyenyekevu na mwenye heshima na ndiyo maana hakusita kufanya naye kazi kwani alijua nia yake ni nzuri.

Hadi sasa, wimbo huo una watazamaji zaidi ya milioni 1.7 ukiwa unashika nafasi ya pili kwenye Mtandao wa YouTube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live