Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Am not single again!

Harmonize Phiona Harmonize na Phiona

Wed, 10 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maaufu wa Bongo Fleva, Harmonize kupitia ukarasa wa akaunti yake ya Instagram amefunguka kuwa kwa sasa yupo tena kwenye mahusiano mapya na amejidhatiti katika hilo baada ya kutowepo kwa muda mrefu katika mahusiano tangu alipoachana na mpenzi wake wa zamani Kajala Masanja.

Harmonize kwa siku za karibuni amekuwa aki-post matukio yakiashiria yupo na mdada mrembo anayefahamika kama “PHIONA”, awali ameeleza kwa kumsifu mwanamke huyo, halafu akaahidi kuchora tattoo yenye sura ya mrembo huyo kama ya mwisho na kisha akaujuza umma kuwa kwa sasa hayupo “SINGLE AGAIN”.

Akiendelea kutikisa charts za Majukwaa mbalimbali ya Muziki Kimtandao Duniani kupitia ngoma yake ya Single Again, kwa jinsi anavyounganisha matukio huenda wimbo wake ukasikilizwa zaidi na zaidi kwani hata hivyo umeshawafikia wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live