Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Akaunti yangu ilisoma zero sababu ya kumpenda, lakini niliachwa!

Kajala Harmonizeee Harmonize na Kajala

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Harmonize amesema alitumia pesa zake nyingi kumhudumia aliyekuwa mpenzi wake, Kajala Masanje na mwisho wa siku akamuacha na penzi lao likafa.

Harmonize amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuweka bango barabarani akidai kuwa sasa hana mpenzi, yupo single baada ya kuachana na Kajala.

Ameandika Harmonize; "Nakumbuka siku moja akaunti yangu ya benki ilisoma zero "0000" kwa sababu ya kumfanya mtoto wa mtu awe na furaha lakini haikusaidia niliachwa.

"Kwa sasa nayachukia sana mapenzi na nimeamua kuwa single japo kuna watoto wa kike wengi wananipenda na wanataka kuanzisha mahusiano na mimi," ameandika Harmonize kwenye Instagram stori yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live